Muziki, Maadili na Uislamu: Mapambano ya Muislamu Anayependa Ukweli

Kabla kuingia uislamu nilizoea kuona wasanii waislamu na tuliona ni kama kawaida kusikiliza nyimbo zao. Wakati huo sikujua mafunzo ya dini, tena nilipenda sana muziki za kila aina. Singeweza kuandika bila muziki. Nilipokuwa nafanya kazi mtandaoni nilihisi tupu bila kuweka muziki. Na ilikuwa kawaida kwangu. 

Baadaye niliingia uislamu kitu cha kushangaza ni kwamba nilikuwa nasoma Qur'an karibu kila wakati mpaka hamu ya muziki ulipungua. Sikuwa na habari ya mafunzo ya dini kupinga muziki. Kupata mafunzo hayo, nilianza kufikiria. Mbona dini inakataza muziki? Na mbona kuna wasanii wanaojitambulisha kama waislamu? Hawa wasanii ni maarufu kwa makafiri na waumini na kwa vile ni waisilamu wanajua ya kwamba muziki ni haramu. Mbona wanazidi kuimba? Nilipoona hadi waislamu wanasikiliza na ni mashabiki wa hawa wasanii ilikuwa mambo ya ajabu kwangu. Mtu anawezaje kujikita muislamu, na kutengeza muziki hasa kuimba mambo machafu? Wanapohitajika kulipa zakat, pesa halali watatoa wapi, kama muziki tayari ni haramu na pesa wanaopata kutoka usanii ni haramu? Mpaka kuona hawa wasanii wanaposema wamefunga ramadhani kisha baada ya idi ndio hawa kama kawaida. Yaani hawaogopi? 

1. Hadithi za Mtume Muhammad (SAW) Kuhusu Muziki

Hadithi kutoka kwa Sahih al-Bukhari: Mtume Muhammad (SAW) alisema:
"Baadhi ya watu watakuwa na vyombo vya muziki na nyimbo katika nyakati za baadaye, na Allah atawalipa adhabu kwa kuwaachia katika dhambi."
(Sahih al-Bukhari, Kitabu cha Meno, Hadithi 5590)

Hadithi hii inadhihirisha kuwa muziki, hasa ule unaohusisha burudani zisizo za kimaadili, unaweza kuleta madhara kwa watu na kuwa chanzo cha kuingilia maadili ya Kiislamu. Kwa hivyo, muziki unaochochea vurugu au unyanyasaji ni jambo ambalo linakataliwa katika Uislamu.

Unaweza je kujua dini yako, kujiita muislamu kisha kuamua usanii na kuimba nyimbo za uzinzi, kushangilia mihadharati na kutokuwa na maadili? Vijana hawataki kuwachapa nyuma na kufuatilia mtindo. Kuna wasanii maarufu ambao vijana wanathamini. Wengi wao wanahusika na mihadharati na kudhulumu watoto wakike kingono. Kwa mfano R Kelly alijulikana jinsi alivyo wazazi wa waathirika walifichua yale waliyokuwa wanayafanya ili kupata mabinti hao na kuwaokoa. Baada ya hayo yote, R Kelly alihukumiwa na kufungwa gerezani. Wangapi bado wako huru? Na wanaendelea na vituko vyao hadi ile siku watapatikana. Zingatia vijana. Wanashawishiwa na uchafu na kutokuwa na maadili. 

Hadithi nyingine kutoka kwa Sahih al-Bukhari: Mtume (SAW) pia alisema:
"Katika umma wangu, kutakuwa na watu ambao watahalalisha uzinzi, pombe, na vyombo vya muziki."
(Sahih al-Bukhari, Kitabu cha Vitu vya Haramu, Hadithi 5591)

Siku hizi wafu huona aibu kujivunia dini yao. Kuonekana sana inawapa aibu na wanahofia kupoteza marafiki. Hasa kwa wanafunzi katika chuo kikuu na shule ya pili. Bado hawajijui vizuri na msanii yeyote anaweza kuwashawishi kwa mambo yasiyofaa muislamu. Ndio kwa maana wengi wanaondoka dini. Wanahisi dini ina kikwazo na wamepotea na starehe ya dunia. Kua na subira kwa hali ya maisha inaleta changamoto kwa vijana.

Katika hadithi hii, muziki umejumuishwa na mambo ambayo Uislamu unakataza, kama vile pombe na uzinzi, kwani yote haya yanaathiri tabia ya mja na kuzuia kumtii Allah. Hii inadhihirisha kuwa muziki unaweza kuwa chanzo cha maovu na kuvuruga maadili ya Kiislamu.

2. Aya za Qur'an Kuhusu Muziki na Uvunjaji wa Maadili

Katika Qur'an, hakuna aya inayozungumzia moja kwa moja muziki, lakini kuna aya nyingi zinazohusiana na mambo yanayoweza kuvuruga maadili, kama vile vitu vinavyohamasisha shauku, dhambi, au mambo yasiyokubalika kwa Uislamu.

Wasanii huimba mambo ya mapenzi na tunajua kwa dini ndoa ndipo sahihi sio uhusiano kinyume na sheria. Kusikiliza muziki huleta hisia za kimapenzi na msikilizaji anaweza kuamua kutekeleza hisia zake wakati hisia za zinaa zinamtawala. Madhara yake ni mimba ya mapema na kuambukizwa na virusi vya ukimwi na maradhi mengineyo. Tayari wanawake wasiokuwa na waume lakini ni wazazi wanabaguliwa. Haikosi kuleta kiwewe kama ni wewe huna mme, watoto ndio hawa na una upekee unahitaji mme, lakini hawapo tarayi kuoa yule aliyekuwa na watatoa wa mwanaume mwingine. Laiti tungehifadhi maadili ya kislamu kusingekuwa na watoto bila wazazi wote wawili. Ni kweli kuna wajane waliokuwa wazazi pia, sipingi. Shida ni kwamba vijana kutokuwa na maadili wanaishi vibaya hadi hata wajane wasiokuwa na hatia wanaathirika na ubaguzi na kuonewa na jamii na kujumuishwa pamoja katika kikundi kimoja, licha ya kwamba wote walipata uja uzito kwa njia tofauti. Mwishowe wasio na hatia wanaonekana kutokuwa na maadili. Isitoshe kuwapa msaada ni changamoto maanake wamewekwa pembeni. Kiwewe ya upekee inawasumbua, wakati wanakosewa huruma. Tafakari hayo yote yanasababishwa na muziki.

Aya kutoka Surah Luqman (31:6):
"Na kuna baadhi ya watu wanaonunua maneno ya uwongo ili wayapotoshe kutoka kwenye njia ya Allah bila kujua, na wakicheka kwao. Hawa ndio watakao pata adhabu ya kudumu."

Katika tafsiri ya aya hii, baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa "maneno ya uwongo" yanaweza kumaanisha muziki na nyimbo ambazo haziendani na maadili ya Kiislamu. Muziki ambao unachochea hisia za dhambi na unazuia kumkumbuka Allah unaweza kuingizwa katika maana hii.

Aya kutoka Surah Al-A'raf (7:31):
"Ewe wana wa Adamu, chukueni mapambo yenu kwa kila masjid, na kuliabudu Allah kwa kumcha yeye."

Aya hii inaonyesha umuhimu wa kuwa na adabu na heshima wakati wa ibada. Muziki ambao unaweza kuingilia au kuvuruga utulivu wa ibada na kumcha Allah unakuwa kinyume na mafundisho ya Uislamu. Hii pia inaonyesha kwamba chochote kinachovuruga hali ya roho au kinacholeta shauku zisizo za kimaadili kinapinga adabu ya ibada.

3. Athari za Muziki kwa Afya ya Kiroho na Kimwili

Hadithi kutoka kwa Ibn Qayyim (Rahimahullah):
Ibn Qayyim alielezea katika kitabu chake "Ighathat al-Lahfan" kuwa muziki una athari kubwa kwa roho na akili ya mja. Alisema kuwa muziki huleta msisimko wa kihisia, na katika baadhi ya hali, unaweza kumzuia mja kutii Allah. Pia, anasema kwamba muziki unaweza kuwa chanzo cha kupoteza heshima na kuhamasisha matendo ya dhambi.

Unaposikiliza kuzika ambazo zina kushawishi kuzini, kuingia ulevi, na kua muhuni, itabadili maisha yako na ni wewe mwenyewe utabaki kua mkosefu. Muziki ina uwongo wa kushawishi msikilizaji pole pole hadi aongeze madhambi makubwa ya kupoteza hadi Imani yako. Ni miradi mkuu wa shetani kwa ajili ya nguvu zake kupoteza watu wanaopendelea muziki. 

Hadithi kutoka kwa Imam Al-Ghazali (Rahimahullah):
Imam Al-Ghazali alielezea katika kitabu chake "Ihya’ Ulum al-Din" kuwa muziki unaweza kuathiri moyo wa mja na kumzuia kutoka kwa ibada ya kweli. Alisema kuwa muziki huweza kuchochea hisia zisizozalisha wema, na hivyo kumfanya mja kuwa mbali na kumtumikia Allah kwa dhati.

Huwezi kumtii Mungu kama wapenda maneno ya wasanii. Dini ina usafi ndani yake na muziki unahusika na uchafu wa kila aina. Ndio kwa maana wanaapa sana. Utaweza je kuongea mambo mazuri kama wapenda kusikiliza wasanii wanaposema maneno machafu? Mdomo wako na ulimi uliumbwa kumsifu Mungu na unaposikiliza muziki, yale yanayofuata ni kuapa kama hawa na kuongelea kila kitu kichafu kinachojulikana kwa binadamu. Aibu huna?

4. Uhusiano wa Muziki na Vitu Vingine Vilivyokatazwa

Muziki mara nyingi hujumuishwa na vitu vingine vilivyokatazwa katika Uislamu. Kama ilivyoelezwa katika hadithi za mtume (SAW), muziki unahusiana na pombe, uzinzi, na vitendo vya maovu. Muziki unaweza kuwa na madhara makubwa kwa roho ya mja, kwa sababu unachochea shauku za kimwili na za kijamii ambazo hazilingani na maadili ya Kiislamu.

Hadithi kutoka kwa Ibn Taymiyyah:
Ibn Taymiyyah alisisitiza kuwa muziki unachochea hisia za kimwili na za kijamii ambazo zinatumiwa kuhamasisha matendo ya dhambi. Alisema kuwa mtu anayeshiriki katika muziki anakuwa mbali na njia ya Allah, na anapoteza nafasi ya kuwa na roho safi na ya kumcha Allah.

Kama unataka kua mcha wa Mungu na kufuatilia njia sahihi ya uislamu, mambo ya dunia wacha nyuma. Dunia tutawaachia wengine wakati wa mauti. Na sisi sote tumepangiwa siku ya mwisho. Mazingira wa dunia hauendani na dini maanake shetani na wachawi wake wamesambaa kote ulimwenguni. Alimpa Allah ahadi kwamba ataenda na wengi jahanam. Atakuja kutoka kushoto, kulia, mbele na nyumba. Unapoendelea kwenye njia iliyonyooka, shetani atakuwa hapo kujaribu kupoteza waumini. Imani yako sio mchezo. Imani yako ni kama dhahabu na kifunguo cha kuingia peponi. Kwa hivyo uwe macho. Huna fursa nyingine. 

Comments