Uchaguzi wa Rafiki: Kipimo Cha Imani na Akhera
"Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema."
Ash-Shu'ara 26:83
Napenda sana kutaja hilo dua katika Salah nikiwa katika sujudu. Kitu kilichonifanya kuandika makala huu leo ni kuzingatia urafiki. Wakati unapochagua rafiki, unataka rafiki ya aina gani? Je, ungependa rafiki ambaye anaaminika? Yule ambaye anajua kumsitiri mwenzake na kumpa nasaha?
Unapokaribia marafiki na kupendelea rafika fulani, jua ya kwamba tabia zake zinaweza kuathiri. Hebu fikiria tena kama rafiki yako ni mtu wa kuhimiza uwe mcha wa Mungu au la. Anayekuwa rafiki lazima awe mtu anayekufaidi duniani na akherah. Watu wengi watakuwa wakosefu siku ya qiyama kwa ajili ya kuchagua marafiki wasioweza kuwasadia wala kuwapa manufaa wa undugu na umoja.
Ukabila sio jambo jipya katika taifa letu. Ukabila huletwa na kutofautiana na kuchagua mwenzako ambaye unatoka kabila moja naye dhidi ya wengine licha ya kwamba sisi sote ni wakenya. Kuna mafunzo kuhusu aya hii kama ni kweli ungependa kuunganishwa na marafiki wema. Katika tafsiri ya Ibn Kathir na hususan Imam Al Qurtubi ilikuwa dua ya Ibrahim AS. Alitaja kuwa moja wa kusema ukweli kwenye akherah. Allah alijibu dua yake, na kila mmoja atakayetaka kutuma salawat kwa Mtume swala Allahu alayhi wa salem ni kutimiza dua ya Ibrahim AS kwa kua hanafi kwa maana hakuwa qaum ul mushrikin.
Tafuta rafiki ambaye atakufanya kua karibu na Allah. Tafuta mtu anayekuhimiza na kupa mawaidha kuendeleza ibada yako. Kama mwenzako wanasababisha uwe mbali na Allah sio sahibu wako bali ni mtihani kwako. Unapoendelea na urafiki isiyokuwa na manufaa mwenye akherah utaona madhara yake. Utajikita huna hamu na ibada tena ibada itakuwa mzito kwako. Kwa maana rafiki asiyekuwa mwema anaweza kufanya uwe na shaka na kupuuza ibada. Uliumbwa kuabudu Allah pekee. Kama rafiki zako hawana manufaa katika maisha yako hasa kwa akherah yako, hakuna haja ya kubaki nao. Itakulazimu kubadili marafi wanaojua umuhimu wa mtihani wa maisha tuliopewa na Mwenyezi Mungu.
Ningependa kula mfano na kisa cha ukweli nami nilishuhudia mwenyewe. Kuna kijana fulani mwanafunzi katika chuo kikuu alikuwa amepotea na maisha ya dunia. Kazi yake ilikuwa kufuatilia wasichana na kulewa kila wakati. Alijaribu kuhusiana bila kufanikiwa. Marafiki walikuwa walevi kama yeye, lakini walikuwa wanapata wasichana wa starehe tu, kama vile vijana hufanya mambo mengi wanaposoma katika chuo kikuu maanake hawawezi kusoma bila kua na wakati wa kukutana kama marafiki baada ya masomo kwa siku. Ndugu huyo alikuwa na changamoto ya kua na marafiki wakweli. Bora alikuwa na watu wa kulewa naye, aliona kuna urafiki hapo. Wakati mwingine walipenda kumkosoa, kumkejeli na kumdhihaki hadi mwenyewe anaondoka na aibu kisha tena alikuwa anazidi kurudi hapo na kulewa nao. Alikuwa na unyongovu na unyongovu lakini marafiki hawakuwa na habari wala kumshughulikia hali yake kiakili. Naye hakujua jinsi ya kujieleza na hakuwa na rafiki wa kweli.
Alianza kunywa pekee yake. Alipokuwa nao wakati mwingine, pia masaa za usiku alikuwa anakunywa pekee yake hadi alijulikana kama mlevi wa eneo hilo. Siku moja alikuwa na kulewa, kawaida kwake. Lakini alikuwa na tabia tofauti kulingana na mashahidi waliomuona ile siku. Kwa bahati mbaya aliteleza na kuangukia mtaro na tayari alilewa, kwa hivyo alikuwa dhaifu sana kuinuka. Kile kilichotokea, alihisi kichefuchefu na kumbuka kwamba alikuwa pekee yake na alitaanguka kwa mgongo wake. Alianza kutapika na kujitapikia maanake alikuwa dhaifu sana kugeuka. Wale waliomuona walimpuuza kama kawaida. Walidhani ni kulewa kwake kawaida kama kila siku, kwa hivyo walitembea mbele na kuwacha kijana akiwa chini kwa hali hiyo. Jambo la kusikitishwa ni kwamba alinyongwa na matapiko. Mwili wake ulipatikana mapema asubuhi. Nilipoitwa kuthibitisha kwamba namjua, nina lake ilijulikana. Kikundi hicho kilikuwa sawa baada ya miezi michache. Waliendelea kufuzu na kuajiriwa na kazi rasmi na wengineo wameoa. Marehemu ndio huyo kaburini, na tayari wenzake wameendelea maishani na kumsahau. Hata wale waliodai kua karibu sana naye wameendelea na maisha yao. Ndio vile maisha huenda.
Mbona nakwambia kisa hiki? Maanisha ya kwamba kwa maisha ya muislamu, rafiki yako ni Allah mwenyewe. Allah ni rafiki yako ya kweli. Wengine wanapokuwacha, wanapokuondokea, Allah yu nawe milele. Badala ya kuhimiza ujinga na kujiingiza kwa uhalifu na mihadarati, uzinzi na kadhalika, wangapi wanaona Allah kama rafiki yao zaidi ya kua Rabbul Alamin? Allah Amesema anakupenda kuliko makosa, tena zaidi ya mara sabini. Unapojisumbua na kutafuta marafiki duniani, jua ya kwamba ukiwa karibu na Allah, hayo yatosha. Maanake Allah atakuunganisha na watendao wema. Allah ni mjuzi wa kila kitu. Anajua binaadam ndani na nje. Anayeonesha na yale aliyostiri. Huwa Rabbul ghayb. Atakosaje Kupa rafiki mwema? Kuzungukwa na rafiki wazuri inaathiri pia afya ya akili. Unaridhika na maisha. Mambo ya dunia ni kwa mda mfupi tu. Lakini qaumu Saliheen wanakuhimiza kuendelea na njia iliyonyooka. Wanakuhimiza kua msafi na mkweli kwa uwezo wako maanake binadamu hukosa kua sahihi wakati mwingine. Lakini yule mwema atakurudisha ili usipotee.
Siku ya Qiyama utakapokuwa mbele ya Mungu nyie wawili, utakuwa na raha kwa kumchagua duniani au majuto?
Marejeleo Mengine
"Siku hiyo waliokuwa marafiki wa karibu watakuwa maadui wao wao, isipokuwa wachaMungu."
(Az-Zukhruf 43:67)
"Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli."
(At-Tawba 9:119)
Mtume Muhammad (Swalla Allahu alayhi wa sallam) amesema: "Mtu huwa yuko katika dini ya rafiki yake wa karibu, hivyo basi kila mmoja wenu na aangalie ni nani anayemfanya rafiki wake wa karibu."
(Hadithi - Imepokewa na Abu Dawud, Tirmidhi)
Katika Hadith Qudsi, Allah anasema: "Mimi ni kama mja wangu anavyonidhania. Niko pamoja naye anaponikumbuka..."
(Imepokewa na Bukhari na Muslim)
"Hakika wale wanaosema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu, kisha wakanyooka, Malaika huwatelemkia wakisema: Msiogope wala msihuzunike, na furahini kwa Pepo mliyoahidiwa."
(Fussilat 41:30)
Mtume (Swalla Allahu alayhi wa sallam) pia amesema: "Mfano wa rafiki mwema na rafiki mbaya ni mfano wa mbeba misk (manukato) na mtu anayepuliza tanuru ya chuma. Mbeba misk atakupa au utanunua kutoka kwake au utapata harufu nzuri, na yule wa tanuru ya chuma atakuchoma au utapata harufu mbaya."
(Imepokewa na Bukhari na Muslim)
Comments
Post a Comment